Aug 4, 2013

WAISLAMU WAHIMIZWA KUFUTURISHA;


 Sheikh.Ramadhan Kwangaya akihutubia muda mfupi kabla ya kufuturu.
  • LENGO NI KUWAONDOSHEA HISIA ZA UNYANYAPAA WAJANE NA YATIMA.
  • WALIOHUDHURIA WARIDHIKA NA HUDUMA.
  • WASHAURI TAASISI IUNGWE MKONO.
Na mwandishi wa munira.
Waislamu nchini wametakiwa kuwa na tabia ya kufuturu pamoja na watu wasiojiweza ili kuwaondelea hisia za kutengwa na jamii.

Wito huo umetolewa jana na Sheikh Ramadhan Khamis Kwangaya katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na taasisi ya Munira Madrasa And Islamic Propagation Association.

Amesema tukio hili lililo fanywa na ndugu zetu wa munira la kuwakusanya wajane,wazee,yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu,ni tukio la kiislamu lakini pia ni tukio la kibinaadamu ambalo tunapaswa kuliiga.

"Ni kweli katika kipindi hiki watu mbalimbali wanawasaidia wasiojiweza,lakini hawakai nao pamoja wakafuturu nao.sasa ndugu zetu mbali ya kuwapa misada lakini leo wametuita na sisi ili kwa pamoja tufuturu nao kwa nia ya kuwafariji,kwa hakika ni jambo la faraja".alisema


kwa upande wake Bwana Sunubi mkazi wa magomeni maeneo ya moroko Hotel amesema "nimefuhishwa sana kwa tukio hili ambalo kimsingi sijawahi kuliona (si maanishi kwamba wengine hawafanyi,la hashaa ila kwa mimi ndiyo kwanza naliona),lakini pia na wapongeza licha ya kuandaa futari mzuri na zenye kupendeza lakini mumeweza kuuridhisha umma huu ulifurika,mungu awape malipo mwema",mwisho wa kumnukuu.


Naye Waziri Muhammed mkazi wa Magomeni Kimamba amesema "kwa hakika munastahiki kuungwa mkono kwa mazuri munayoyafanya,nimefurahi na nimeridhika na huduma na utendaji wenu".alisema


katika futari hiyo iliyopewa jina la MUNIRA FAMILY DAY,ilifanyika jana na kuhudhuriwa na mashekh na watu mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali.


Kabla ya kufuturu paliswaliwa Swala ya Maghrib katika uwanja huo huo Swala ambayo iliongzwa na Sheikh Abdallah Haroun Nyumba kutoka Mbagara jijini Dar es salaam>

Huu ni mwaka wa tano mfululizo kwa taasisi hii kuandaa futari ya pamoja ambapo kila mwaka idadi ya wanohudhuria futari hiyo inapanda na mwaka huu inakadiriwa watu mia mia tano walihudhuria futari hiyo.

 HAWA NI WATOTO AMBAO MIONGONI MWAO NI YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU WAKIWA WAMEHUDHURIA KATIKA FUTARI YA PAMOJA ILIYOANDALIWA NA TAASISI HII.

 HAWA NI SEHEMU YA AKINA MAMA AMBAO MIONGONI MWAO NI WAJANE NAO WAKIFUTURU WAKATI PAKIADHINIWA

SEHEMU YA WAUMINI WAKISWALI SWALATUL MAGHRIB KATIKA HAFLA YA FUTARI YA PAMOJA ILIYOFANYIKA JANA.
 KULENI PAMOJA WALA MUSITENGANE" HAYA NI MANENO YA MTUME S.A.W..KWA HAKIKA KUFUTURU PAMOJA NI RAHA.