Idadi ya waliopoteza maisha baada ya jengo lenye ghorofa 5
kuporomoka katika mji mkuu wa kibiashara wa Nigeria, Lagos imepindukia
30.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nigeria imesema kuwa, jengo
hilo ambalo lilikuwa linaendelea kujengwa liliporomoka Jumanne
iliyopita, kutokana na ukiukaji wa kanuni za ujenzi. Imesema kuwa, jengo
hilo liliporomoka baada ya mmiliki wake kuamua kuongeza ghorofa za
ziada pasina idhini ya mamlaka husika. Awali iliripotiwa kuwa watu 4 tu ndio waliokuwa wameaga dunia katika mkasa huo lakini kufikia jana jioni baada ya shughuli za kupekua vifusi kukamilika, miili zaidi ilipatikana.
Aidha watu 13 walipatikana wakiwa hai katika shughuli hizo jana Jumatano.
Taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nigeria imemtaka mmiliki wa jengo hilo kupiga ripoti mara moja katika kituo chochote cha polisi la sivyo mkono wa sheria utafuata mkondo wake.
0 comments:
Post a Comment