Jan 2, 2014

Jeshi la Misri laendelea kupigana na waandamanaji

Jeshi la Misri laendelea kupigana na waandamanaji







Vikosi vya usalama vya jeshi la Misri vimeendelea kupigana na waandamanaji wanaopinga jeshi na kuondolewa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Muhammad Mursi.

Waandamanaji wawili wameripotiwa kuuawa katika machafuko yaliyotokea kati ya waandamanaji wanaounga mkono harakati ya Ikhwanul Muslimin na vikosi vya usalama kwenye mji wa Alexandria. 

Machafuko kama hayo pia yameripotiwa katika mji wa Nile Delta na mji mkuu, Cairo.

 
Hayo yanajiri huku Amir wa Qatar akituhumiwa na serikali ya mpito ya Misri kuunga mkono kundi la Ikhwnul Muslimin na kuwapa hifadhi viongozi wa kundi hilo. Miezi kadhaa baada ya jeshi kupindua serikali ya Muhammad Musri, serikali ya mpito ya Misri imechukua hatua tofauti ili kulifuta kundi hilo kubwa la kisiasa na hata kulitangaza kuwa ni la kigaidi.

0 comments:

Post a Comment