Mar 10, 2016

Upinzani wasusia duru ya pili ya uchaguzi Niger

Vifaa vya uchaguzi viliopigwa picha wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais mjini Niamey, Februari 21, 2016.
Vifaa vya uchaguzi viliopigwa picha wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais mjini Niamey, Februari 21, 2016.

Muungano wa upinzani nchini Niger, Copa 2016, unaomuunga mkono Hama Amadou ambaye angelishindana na Rais anayemaliza muda wake Mahamadou Issoufou umesema Jumanne 8 Machi mjini Niamey kuwa umesisitisha kushiriki katika mchakato wa uchaguzi.

Hayo yanajiri wakati duru ya pili ya uchaguzi wa urais imepangwa kufanyika Machi 20.

Muungano wa vyama vya upinzani umechukua uamuzi huo kufuatia kasoro nyingi uliogundua tangu duru ya kwanza yauchaguzi wa urais. Upinzani unalaani nia ya Rais Issoufou ya kutaka kupata ushindi kwa nguvu, amesema msemaji wa muungano wa vyama vya upinzani Seyni Oumarou katika taarifa yake.

Ametetea uamuzi huu kutokana na kukosekana kwa "tangazo rasmi" la matokeo ya duru ya kwanza ya tarehe 21 Februari na "kutotendewa haki sawa kati ya wagombea wawili" katika uchaguzi wa urais. Mpinzani mkuu wa Mahamadou Issouffou, Hama Amadou anazuiliwa kwa sasa katika kesi yenye utata wa biashara ya watoto.

Mahamadou Issoufou, ambaye anawania muhula wa pili, alipata katika duru ya kwanza 48.43% ya kura mbele ya Hama Amadou aliyepata17.73% katika uchaguzi uliokosolewa na upinzani, uchaguzi ambao utawala ulisema ulikua wa wazi.Muungano wa vyama vya upinzania COPA 2016 pia "unaomba" watu waliochaguliwa kwa niaba ya muungano huo "kusitisha shughuli zote" katika Bunge na kwa wawakilishi wake "kuondoka kwenye Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi(CENI). "

0 comments:

Post a Comment