Kwa mara nyingine Sheikh Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha
al-Azhar nchini Misri ametaka kufanyika kikao cha pamoja baina ya
maulama wa Kishia na Kisuni kwa lengo la kuimarisha umoja baina yao.
Sheikh Ahmed el-Tayeb ameyasema hayo alipokutana na Rais Fuad Masum
wa Iraq na ujumbe wa ngazi za juu alioongozana nao mjini Cairo, Misri.
Katika mazungumzo yao kwa mara nyingine Sheikh el-Tayeb amesisitizia umuhimu wa kufanyika kikao hicho baina ya maulama wa Kisuni na Maraajii wa Kishia, lengo kuu likiwa ni kudumisha umoja ndani ya umma wa Kiislamu.
Amesema kuwa, Iraq ni nchi kubwa katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu huku ikiwa na nafasi maalumu katika moyo wa kila mtu Mwarabu na Mwislamu duniani.
Sheikh mkuu huyo wa chuo kikuu hicho cha Kiislamu nchini Misri ameongeza kuwa, al-Azhar iko tayari kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za kila upande nchini Iraq katika kukabiliana na aina yoyote ya njama za kuibua tofauti na mifarakano baina ya Waislamu.
Kwa upande wake Rais Fuad Masum wa Iraq sanjari na kukaribisha pendekezo hilo, amesisitizia udharura wa kuongezwa kiwango cha ushirikiano wa nchi mbili, za Iraq na Misri.
Safari ya rais wa Iraq nchini Misri imefanyika kufuatia mwaliko wa serikali ya Cairo ambapo pia Rais Masum amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Abdel Fattah el-Sisi na kujadiliana naye masuala mbalimbali.

0 comments:
Post a Comment