Aug 14, 2014

UN yatangaza hali ya tahadhari Iraq


Baadhi ya wakimbizi kaskazini mwa Iraq

Umoja wa Mataifa umetangaza hali ya tahadhari ya kiwango cha juu zaidi cha dharura kwa watu milioni moja unusu nchini Iraq kufuatia wapiganaji wa kiislamu wa Islamic State kaskazini mwa Iraq.

Umoja wa mataifa unasema kuwa utatoa msaada zaidi kwa wakimbizi ambao wamefanikiwa kukimbia kutoka mlima sinjar na wairaq wengine 400,000 ambao wamekimbilia maisha yao kwenye mkoa wa wakurdi wa Dohuk karibu na mpaka na Uturuki.

Wakuu wa jimbo hilo la Kurdistan wamesema hali kwenye jimbo la Dohuk lililo na wakimbizi 15000 ni mahututi na majeshi ya Marekani hayana mpango wa kuwaokoa.

Syria,Sudan Kaskazini na Jamhuri ya Afrika ya Kati ni mataifa mengine yanayohitaji misaada kwa dharura .

Mwakilishi wa UN Nickolay Mladenioy amesema kuwa Tangazo hili linapelekea kuongezwa kwa rasilimali kwa mizigo,fedha na mali ili kuhakikisha mahitaji ya walioadhirika
Maelfu ya wakimbizi wamekwama milimani bila maji wala chakula

Maelfu ya watu hasa wakristo na jamii ya Yazidi walitorokea mlimani baada ya kutoroshwa makwao.

Mwandishi wa bbc mjini humo Frank Gardner anasema kuwa walilazimika kuchukua hifadhi kwenye maghala yasiyikuwa na maji wala usafi.

Zaidi ya watu milioni moja wakiwemo wa jamii ya Yazidi na dini zingine ndogo wamelazimika kuhama makwao tangu wanamgambo wa Sunni wa Islamic State kuyadhibiti maeneo ya kaskazini mwa Iraq mwezi Juni.

Maafisa wa wa Kurdi wanasema kuwa hali kwa sasa ni mbaya wakimbizi wanahitaji kwa dharura mahema, chakula na maji.

0 comments:

Post a Comment