Ile kauli kwamba umoja ni nguvu jana ilidhihirika pale waislamu walipoamua kutumia umoja wao na kuiokoa nyumba ya ALLAH.
Moto
huo uliodumu takriban masaa matatu huku makampuni ya uokoaji
yakipambana kuuzima moto na kukutana kikwazo cha kuishiwa maji mara kwa
mara kuliwapelekea waislamu kuchukua maamuzi busara.
Maamuzi hayo yaliyofanyiwa kazi kivitendo ndiyo yaliyoweza kufanikiwa kuuzima moto huo kwa UWEZO WA ALLAH.
Walilazimika kubeba maji kwa kutumia ndoo na kuyaingiza maji katika magari ya zima moto na zima moto kuyafanyia kazi.
Lakini wengine walichukua maji na kwa ujasiri waliweza kupambana na moto kwa kuuzima bila ya kutumia magari ya uokoaji.
Hata baada ya kufanikiwa kuuzima waislamu walionekana kupongezana kwa furaha.
"hiili
ni fundisho,ni dhahiri sisi waislamu tukiondoa tofauti zetu na
tukashirikiana kwa nguvu moja ni lazima tutapata mafanikio" alisikika
akisema mtu mzima.
Msikiti wa mtambani ni msikiti kinara wa kuzungumzia bila ya woga dhulma inayofanywa na serikali dhidi ya waislamu.
Hadi sasa haijafahamika rasmi hasara iliyotokana na moto huo ila mabweni yote ya wanafunzi yametekea.
Sehemu ya chini ya msikiti huo umenusurika.
SEHEMU YA WATU WAKISHUHUDIA TUKIO HILO.
MOJA YA MAGARI YA UOKOAJI MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKA ENEO LA TUKIO.
WAISLAMU WAKIPANDISHA MAJI KATIKA GARI LA ZIMA MOTO BAADA YA GARI HILO KUISHIWA MAJI.
WANAUSALAMA WAKIWA ENEO LA TUKIO.
MSIKITI UKISHIKA MOTO NA HIYO NI SEHEMU YA SHULE IKIUNGUA.
WAISLAMU WAKIZIMA MOTO KWA KUTUMIA MAJI
WAKIWA WAMEPANGA SWAFU KUPEANA NDOA ZA MAJI ILI KUYAFIKISHA SEHEMU HUSIKA
GARI LIMEISHIWA MAJI NA WAISLAMU WANAINGIZA MAJI KATIKA GARI LA ZIMA MOTO
NI KWELI JUHUDI YA DHATI ALLAH UINGA MKONO
Aug 14, 2014
SHUHUDIA WAISLAMU WALIPOAMUA KUUZIMA MOTO KATIKA MSIKITI WA MTAMBANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment