Na mwandishi wa munira kutoka Kilimanjaro.
Waalimu wa madrasa nchini Tanzania
wametakiwa kuwa na umoja baina yao
ili kujenga heshima.
Hayo yamesemwa na DR. HUSSEN RAMADHAN MBEZI Afisa mnadhim mkuu wa Jeshi la Polisi nchi Tanzania ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika
mashindano ya kuhifadhi Qur aan yaliyofanyika Himo Mkoani Kilimanjaro mwishoni
mwa wiki iliyopita.
Amesema bila ya umoja wa kweli kwa waalimu wa madrasa,itakuwa
vigumu kupata mafanikio,
“Kwa kweli ndugu
zangu waalimu munafanya kazi kubwa sana,hawa watoto wamehifadhi kutokana na
juhudi zenu,mimi naamini kabisa kama mutakuwa na umoja wa kweli mukafanya mambo
kwa umoja,basi milango ya mafanikio ipo wazi kwenu kwa uwezo wa ALLAH S.W.”
Habari hizi ni kwa mujibu wa mwakilishi wetu wa munira(Ustaadh Omar Awadh Msuya) wa Kilimanjaro.
Enter your comment...mashallah ni jambo la kheri hilo allah awazidishie katika amali zenu njema
ReplyDelete