Askari
wa Kikosi cha Zima moto na Uokoaji Wakiwa wamepanda juu ya Mnara wa Simu
Uliopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam Muda mfupi uliopita kwaajili ya
kumuokoa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Hassan Ambaye
alipanda juu ya mnara huo kwa lengo la kufikisha Ujumbe wa kutaka
kuonana na Raisi Kikwete ili aweze kumwelezea kwa kile anachodai kuwa
jeshi la polisi lilimbambikia kesi na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha
Miaka 6 kwenda jela
Kijana
aliyefahamika kwa jina moja la Hassan akiongea na waandishi wa habari
mara baada ya kushushwa juu ya Mnara wa Simu na Askari wa Kikosi cha
Zimamoto na Uokoaji,Ubungo jijini Dar
Gari la Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji likiwa limetia timu eneo la tukio kwa ajili ya Kuokoa
Wakazi wa
Jiji la Dar wakishuhudia gari la Polisi likiondoka na Kijana Hassan
ambaye alipanda juu ya Mnara, Ubungo jijini Dar Es Salaam
0 comments:
Post a Comment