Mashambulio ya wanamgambo wa kundi
la waasi wa LRA la nchini Uganda yanazidi kupamba moto siku hadi siku
huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Taarifa zinasema kuwa, kundi la waasi wa
LRA la nchini Uganda kwa miaka kadhaa limekuwa likitekeleza mashambulio
na kufanya mauaji huko kaskazini mwa Uganda, Sudan Kusini, na Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo, na hivi sasa limejizatiti katika eneo la
kusini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Kiongozi mmoja wa Asasi
ya Kiraia katika Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema kuwa, kila wiki
wanamgambo wa LRA wanavishambulia vijiji, wanafanya mauaji, ubakaji,
uporaji na kuwateka nyara wenyeji wa eneo hilo.
Ripoti ya Umoja wa
Mataifa inaonyesha kuwa, kundi la LRA limeshauwa zaidi ya watu laki moja
katika eneo la katikati mwa Afrika katika kipindi cha miaka 27
iliyopita.
Kundi hilo pia linatuhumiwa kuwateka nyara zaidi ya watoto
elfu sitini.
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC inamsaka Joseph Kony
kiongozi wa LRA na baadhi ya wasaidizi wake kwa kutenda jinai za kivita
na zilizo dhidi ya binadamu.
0 comments:
Post a Comment