Spika wa Majlisi ya Ushauri wa
Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kukaliwa kwa mabavu Palestina ndio kadhia
kubwa kabisa katika ulimwengu wa Kiislamu.
Spika wa Bunge la Iran amesema kuwa, ili
kukabiliana na adui wa pamoja kuna haja ya kuweko ushirikiano wa kila
upande wa Waislamu sambamba na kulinda umoja na mshikamano baina yao.
Spika Larijani ameeleza kusikitishwa kwake na jinsi ulimwengu wa
Kiislamu hivi sasa ulivyokumbwa na makundi mabaya ya kufurutu ada ambayo
yamekuwa yakikuza hitilafu ndogo zilizoko baina ya Waislamu na hivyo
kufanya njama za kuvuruga umoja miongoni mwa Waislamu.
0 comments:
Post a Comment