Kampeni ya kimataifa ya kuususia
utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na jinai na mauaji ya kinyama
uliofanya katika vita dhidi ya Ukanda wa Gaza inazidi kupata nguvu kwa
kutolewa wito wa kufanikisha kampeni hiyo kutoka pembe mbali mbali za
dunia.
Harakati inayojulikana kama Ususiaji, Upunguzaji na Uwekaji
Vikwazo (BDS) imesisitiza kuendeleza kampeni hiyo ikiamini kwamba njia
kuu ya kukomesha jinai na uchokozi wa Israel dhidi ya Palestina ni
kuususia utawala huo haramu.
Katika upande mwengine wananchi wa Jordan
wametoa wito wa kususiwa bidhaa za utawala wa Kizayuni kutokana na
mashambulio yake ya kinyama dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
Chama cha Wafanyabiashara na waagizaji bidhaa nchini Jordan kimetoa wito
wa kususiwa bidhaa na bandari za Israel ikiwa ni hatua ya kulalamikia
jinai za utawala huo ghasibu dhidi ya wakaazi wasio na ulinzi wa Ukanda
wa Gaza.
Wakati huohuo wajumbe wa vyama vya wafanyabiashara, viwanda na
kilimo huko Palestina wamezitaka sekta za biashara na viwanda kuingiza
bidhaa za Jordan katika masoko ya Palestina badala ya bidhaa za Israel…/
0 comments:
Post a Comment