Rais kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini muda mfupi baada ya kuwaswali swala ya eidd katika msikiti wa upanga jijini Dar es salaam
Waislamu kote duniani leo wameswali Sala ya Idul Fitr na kusherehekea sikukuu hiyo adhimu, baada ya kuumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani hapo jana.
Sala ya Idul Fitr mjini hapa tanzania ambayo imefanyika muda mfupi uliopita, inasaliwa katika misikiti na viwanja vya wazi mbalimbali.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu katika nchi mbalimbali walianza kusherehekea Sikukuu ya Idul Fitr tokea jana.
Wakati huohuo, Rais Hassan Rouhani amewatumia salamu za mkono wa Idi Waislamu wote ulimwenguni na hasa wananchi wa Iran, baada ya kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
kwa upande wake Rais Rouhani wa Iran amesema kuwa, wakati Waislamu katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani wameshuhudia mauaji ya kinyama yakifanywa na Wazayuni maghasibu dhidi ya Waislamu wasio na hatia wa Ghaza na hali kadhalika chokochoko vita vya kikabila na kidini zinazofanywa na maadui wa Uislamu dhidi ya Umma wa Kiislamu, njia pekee za kurejesha amani na utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati na kukabiliana na njama za maadui, ni kuwepo umoja na mshikamano katika Umma wote wa Kiislamu.
taasisi ya munira madrasa kupitia blog hii inatoa mkono wa heri na fanaka kwa Waislamu wote ulimwenguni na, kwa mnasaba huu wa kusherehekea sikukuu ya Idul Fitr.

0 comments:
Post a Comment