Jul 29, 2014

Waislamu Kenya waadhimisha Idul-Fitr

Waislamu nchini Kenya leo Jumatatu wamejiunga na wenzao katika nchi kadhaa duniani kuadhimisha sikukuu ya Idul-Fitr inayoashiria kumalizika mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

Sala ya Idd imesaliwa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo huku Waislamu wa jijini Nairobi wakikusanyika katika uwanja wa Sir Ali kwa ajili ya ibada hiyo. 

Sheikh kuu wa msikiti wa Jamia, Muhammad Swalihu, amesema japo Wakenya wanasherehekea iddi kwa furaha lakini Wapalestina wanaadhimisha siku hii chini ya madhila na manyanyaso makubwa kutoka kwa utawala ghasibu wa Israel.

 Kiongozi huyo amesema watu wa Palestina ambao ndio walio katika haki watapata ushindi dhidi ya wazayuni maghasibu. 

Punde baada ya Sala ya Idul-Fitr huko Nairobi, Waislamu walifanya maandamano huku wakitoa nara za kulaani jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza

0 comments:

Post a Comment