Taasisi ya Munira Madrasa yenye makazi yake Jijini Dar es salaam,hivi karibuni ilifanya futari ya pamoja na kuwashirikisha watu mbalimbali.
Futari hiyo iliyowajumuisha wanafunzi,wazazi na waalimu wa madrasa hiyo iliweza kuwapa fursa ya kufuturu pamoja na wajane,yatima,wazee na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Akiongea na mwandishi wa habari hizi,muda mfupi baada ya futari hiyo,katibu mkuu wa Taasisi hiyo Ustaadh Juma Rashid mbali ya kuwashukuru wote waliochangia,alisema "tumeaamua kuwaalika wajane,yatima,wazee na watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa lengo la kuwafariji,ili wasihisi kwamba wanatengwa"
Aliongeza kusema ni "utaratibu wetu sisi munira madrasa kila mwaka inapofika jumamosi ya pili ya kumi la pili kufuturu pamoja futari ya wazi sisi na hawa wajane yatima,wazee na watoto waishio katika mazingira magumu,ndiyo maana tukaiita siku hii kuwa ni MUNIRA FAMILY DAY"mwisho wa kumnukuu.
Sehemu ya futari hiyo ilichangiwa na Al Baraka Foundation na Zanzibar Insurerance Cooperation.
Baadhi ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu wakijumuika katika futari hiyo.
Mhadhiri na imam wa masjid Tawwab ya magomeni makuti Al haj Sheikh Mahmuod Jaji na baadhi ya wazazi wakishiriki katika futari hiyo.
sehemu ya watu waliohudhuria futari hiyo
0 comments:
Post a Comment