Polisi nchini kenya wamemtia
mbaroni gavana wa jimbo la Lamu lililokumbwa na mapigano hivi majuzi na
kusababisha vifo vya watu zaidi ya 65.
Polisi walimshika Issa Timamy,kufuatia tuhuma za kuhusika na mashambulizi yaliyotokea Mpeketoni mapema mwezi huu.
Punde baada ya tukio hilo rais Uhuru Kenyatta alikatalia mbali madai kuwa ilikuwa shambulizi la kigaidi lililotekelezwa na kundi la waislamu la Al shabab.
Kundi la wapiganaji kutoka Somalia Al shabab lilidai kutekeleza shambulizi hilo.
Bwana Timamy ni Gavana wa pekee kutoka chama cha UDF .
Aidha wavamizi waliwalenga wanaume ambao hawakuwa waislamu na kuwataka kukariri shahada ama aya za Quran,wale walioshindwa walikuawa .
Siku ya jumatano maafisa wa utawala katika jimbo hilo la Lamu walidai kuwa wamewakamata watu 13 waliokuwa wakipanga njama ya kufanya uvamizi zaidi.
0 comments:
Post a Comment