Habari kutoka nchini Libya zinaeleza kuwa watu waliokuwa wamejihami na Silaha nzito waliuteka Gari ya Serikali Kibaraka ya nchi hiyo iliyokuwa na Pesa nyingi uliotolewa kama msaada na nchi za Kimagharibi kwa Utawala huo.
Duru zinaeleza kuwa Wanaume kadhaa waliokuwa na Gari ya Kivita waliuteka Gari ya kubebea mzigo uliokuwa na Pesa ya Utawala wa Libyya zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 73 kwenye Barabara inayounganisha Tripoli na Sirta na hatimae Gari hiyo ya Pesa kuelekeza kusikojulikana.
Kamisna Mkuu wa Polisi wa Nchi alithibitisha kutokea tukio hilo na kuongeza kuwa Pesa hizo iliyokuwa unaelekea kwenye Benki kuu ya Libya uliopo mjini Tripoli umetoweka kutoka kwenye mikono yao.
"Wana mgambo waliokuwa na Silaha wameupora Pesa Taslim ya Dola za Kimarekani zaidi Milioni 73 na Polisi wanaendelea na uchunguzi wao na tunasikitishwa na kitendo hicho cha Ujambazi!" alisema Gen:Abdi Fatah. Mohamed.
Katika siku za hivi karibuni kulikuwa na mapambano uliowahusisha baina ya Serikali dhaifu ya Libya na Wapiganaji wa Kislaam wa Ansaru Sheri'ah.
0 comments:
Post a Comment