Dec 1, 2013

HAY ATUL ULAMAA YAENDESHA SEMINA YA MAIMAMU

 Baadhi ya wana semina wakiwa katika makundi kujadili mada mbalimbali.


Taasisi ya HAY ATUL ULAMAA yenye makazi yake jijini Dar es salaam,leo imeendesha semina ya siku moja kwa maimamu wa misikiti.

Semina hiyo ya mafunzo ya uongozi wa misikiti na vituo vya Kiislamu ina lengo la kuwajengea uwezo maimamu  ya kuongoza kwa misingi ya Uwajibikaji.


Akifungua semina hiyo Sheikh Yasir Masoud ambaye ni katibu mkuu wa HAY ATUL ULAMAA amesema msikiti umekuwa ni moja ya taasisi muhimu sana katika jamii ya kiislamu na jamii kwa ujumla.

"Ndugu wana semina hatuwezi kuukwepa ukweli halisi kwamba mfuko wa uzazi wa msikiti umezaa wanawake na wanaume na kuacha athari kubwa ya wanazuoni wakubwa na wakutegemewa hapa Duniani"

Aliendelea kusema kwa sasa inaonekana hali hiyo ni kinyume na imebakia kuwa msikiti ni sehemu ya ibadatu,ni vyema turudishe hadhi ya misikiti"mwisho wa kumnukuu.

semina hiyo ina endelea na inatarajiwa kumalizika leo saa kumi. 

munira blog itawajulisha zaidi kwa yatakayojiri.  
 SHEIKH YASIR MASUOD KATIBU MKUU AKIWASILISHA MADA.








0 comments:

Post a Comment