HII ILIKUWA NI ENZI ZA UHAI WA MTOTO SULEYMAN PALE KUNDI LA WANA MUNIRA MADRASA NA MUNIRA BLOG ILIPOMTEMBELEA KATIKA SIKUKUU YA IDDIL HAJJ KWA LENGO LA KUMFARIJI.
Hatimaye mtoto Suleyman Rajab amefariki dunia.
Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu ni kwamba mtoto huyo amefariki jana majira ya saa moja.usiku
Akiongea kwa njia ya simu mapema leo hii Asubuhi,Bwana Rajabu amesema "nimekukupigia simu kukufahamisha kwamba rafiki yako hatunaye ametutoka dunia"
Akiendelea kumfafanulia mwandishi wa munira blog,bwana Rajabu amesema a"mefia hapa hapa nyumbani (Kivule) na tunatarajia kuondoka hapa saa sita kwenda kumzika maeneo ya maneromango wilaya ya kisarawe mkoa wa Pwani"alisema kwa huzuni.
"Naomba radhi nimechelewa kukufahamisha kutoka na kufazaika,kwani nilipaswa kukufahamisha mapema kutokana na mwenyewe mar hum mara kwa mara akikukumbuka wewe na wanafunzi wako",mwisho wa kumnukuu.
Mtoto Suleiman alikuwa ana sumbuliwa na ugonjwa wa ajabu wa kuvimba mguu kupita kiasi.
Kwa mujibu wa historia yake tangu azaliwa hakuwahi nyayo yake kukanyaga chini.
Hivi karibuni mtoto Suleyman alilazwa katika Hospitali ya CCBRT ya mikocheni ambapo mwishowe madaktari walishindwa kumtibia na kushauri apelekwe nchini india.
Mtoto suleyman amefariki akiwa na umri wa miaka 17 na alikuwa anatarajia kupelekwa inchini india kwa matibabu.
munira blog inawapa pole wazazi,ndugu na jamaa wa mar hum Suleyma,na ina waomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu,INNAA LILLAAH WAINNAA ILAYHI RAAJIUUN
Dec 7, 2013
MTOTO SULEIMAN AFARIKI DUNIA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment