Tunaendelea kuzitaja Faida za kuomba Tobah sehemu ya pili …
5-Kuwekewa Nuru (mwanga) ambao utamulika wenye kuomba tawbah watakapokuwa wanapita katika Siraatw siku ya Qiyaamah.
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا عَسَى رَبُّكُمْ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يَوْمَ لَا يُخْزِي اللَّهُ النَّبِيَّ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ نُورُهُمْ يَسْعَى بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ)
(Enyi
mlioamini! Tubuni kwa Allaah tawbah iliyo ya kweli! Asaa Mola wenu
Mlezi Aakakufutieni maovu yenu na Akakuingizeni katika Pepo zipitazo mito kati yake, siku ambayo Allaah Hatamdhalilisha Nabii na walioamini pamoja naye. Nuru yao inakwenda mbele yao
na pande zao za kulia, na huku wanasema: Mola wetu Mlezi! Tutimilizie
nuru yetu, na Utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila
kitu) [At-Tahriym: 8]
6-Malaika wanawaombea maghfira waumini walioamini na wenye kuomba Tobah
(الَّذِينَ يَحْمِلُونَ الْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ)
(Wale
wanaobeba 'Arshi, na wanaoizunguka, wanamsabihi na kumhimidi Mola wao
Mlezi, na wanamuamini, na wanawaombea msamaha walioamini kwa kusema:
Mola wetu Mlezi! Umekienea kila kitu kwa Rehma na ujuzi. Basi wasamehe
waliotubu na wakaifuata Njia Yako, na waepushe na adhabu ya Jahannam) [Ghaafir: 7]
7- Kubadilishiwa mabaya na kufanywa yawe mema
(إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُوْلَئِكَ يُبَدِّلُ اللَّهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا)
(Isipokuwa atakayetubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Allaah Atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Allaah ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu) [Al-Furqaan: 70]
Baada
ya kujua faida nyingi na fadhila za kuomba Tawbah, je, hustahiki ndugu
Muislamu kupata fadhila hizo adhimu? na nyingi nyinginezo? Kwanini
usitubu ili uzipate? Asiyetaka kutubu baada ya kujua fadhila hizo ajue
kuwa anajizuia na kudhulumu nafsi yake kupata furaha, kufaulu duniani
na akhera na pia kupata Ridhaa ya Mola Wake.
Bila shaka kila mmoja wetu atatamani fadhila hizo na kukimbilia kwa Mola wetu kumuomba Tobah ya Kweli.
0 comments:
Post a Comment