Jumanne, Machi 25.

Dec 8, 2013

WAZAZI MUZITHAMINI SHULE ZA AWALI ZA KIISLAMU


WITO umetolewa kwa wazazi wa Kiislamu kuwapeleka watoto wao katika shule za awali za kiislamu ili kuwapatia maadili mema 

Wito huo umetolewa hivi punde na Sheikh Ramadhan Pazi alipokuwa ana wahutubia wazazi na walezi waliohudhuria mahafali ya tatu ya AMMAR BIN YASIR NURSERY SCHOOL iliyopo Mbagara Dar es salaam.

Amesema umejengeka utamaduni kwa baadhi ya wazazi wa kiislamu kutumia pesa nyingi kwa kuwalipia ada watoto wao wanaosoma shule za awali za kimataifa (Internation School),wakati elimu inayotolewa huko hailingani kwa ubora na elimu za huku.

"Kule wanafuata Kiingreza,lakini nasari zetu za Kiislamu zina Kiingreza,Kiarabu na maadilili na malezi bora ya kiislamu,hii ina maanisha Nasari zetu nii bora kwa hivyo Tuzithamini",alisema.

Awali wanafunzi hao walionyesha uhodari kwa kutaja vitu mbalimbali kwa lugha ya Kiarabu na Kiswahili huku wakisoma Dua kadhaa ambazo waislamu wanalazimika kuzitumia kila siku katika maisha yao.

Jumla ya Wanafunzi k18 walikabidhiwa vyeti kutoka kwa mgeni rasmi baada ya kukhitimu elimu ya awali na kutoa fursa ya kujiunga darasa la kwanza hapo mwakani.

Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Ustaadh Juma Rashid ambaye ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Munira Madrasa And Islamic Propagation Associatin na ndiye mkurugenzi wa Munira Blog.

0 comments:

Post a Comment