Dec 5, 2013

Misri yazuia maandamano ya kura ya maoni ya Katiba

Mkuu wa Usalama wa Umma wa Misri ametahadharisha juu ya kufanyika maandamano ya kupinga jeshi ili kuvuruga kura ya maoni ya katiba mpya. 

Sayyed Shafiq amesema kwamba, jitihada zozote za kuvuruga kura ya maoni zitakabiliwa na hatua kali za kisheria na kwamba hawataruhusu mwenendo huo wa kidemokrasia uvurugwe.

Kura hiyo ya maoni ya katiba mpya ya Misri itafanyika mwezi ujao wa Januari na iwapo itapitishwa itaimarisha nafasi ya jeshi la Misri. 

Pia rasmu ya katiba hiyo ina kipengee kinachopiga marufuku kuasisiwa vyama vyenye mielekeo ya kidini ambayo ilikuwa ikitumiwa katika utawala wa miaka 30 wa Dikteta Hosni Mubarak.

Hayo yanajiri huku msemaji wa tume ya watu 50 iliyotunga katiba hiyo akisema kuwa baada ya kupasishwa katiba mpya haitafanyiwa marekebisho.

0 comments:

Post a Comment