Dec 5, 2013

Libya yaafiki sheria Uislamu katika Katiba

Bunge la Taifa la Libya GNC limepiga kura na kuafiki kuwa sheria za Kiislamu ziwe msingi na kigezo cha sheria zote za nchi hiyo. 
Taarifa na Bunge hilo imeeleza kuwa, tume maalumu itapitia sheria zote za nchi hiyo na kuhakikisha kwamba zinaendana na misingi ya Kiislamu na kwamba sharia itakuwa ndio chanzo cha sheria za Libya.

Uamuzi huo unaweza kuathiri sheria za mabenki, jinai na fedha huku mabadiliko mapya yakitarajiwa kufanywa katika miamala ya kifedha ili kuepusha riba.

Tangu alipopinduliwa dikteta Muammar Gaddafi, Libya kwa miaka miwili sasa imekuwa ikiongozwa na serikali ya mpito lakini bila Katiba. 

Pia kamati ya watu 60 inatarajiwa kupasishwa ili kutunga Katiba mpya ya nchi hiyo.

0 comments:

Post a Comment