Dec 1, 2013

Mahakama Misri yakubali rufaa ya wasichana 21



Majaji nchini Misri wamekubali rufaa ya wasichana 21 waliohukumiwa jela hivi karibuni nchini humo. 

Majaji hao wametangaza kuwa, mahakama ya nchi hiyo itasikiliza upya kesi ya wasichana hao mwanzoni mwa mwezi huu mkoani Alexandria. 

Siku ya Jumatano iliyopita mahakama moja nchini Misri iliwahukumu kifungo cha miaka 11 jela wasichana 14 wanaotajwa kuwa wafuasi wa Harakati ya Ikhwanul Muslimiin  kwa tuhuma za kushiriki katika maandamano dhidi ya serikali na kupambana na wafuasi wanaoiunga mkono serikali ya nchi hiyo. 

Hii ni katika hali ambayo wasichana wengine 18 pia walihukumiwa kifungo jela kwa tuhuma hizo hizo na kwamba wote kwa pamoja watafikishwa katika mahakama hiyo ya rufaa tarehe 7 ya mwezi huu. 

Tayari mashirika mbalimbali ya Kimataifa likiwemo Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International, yamelaani hatua ya kuwatia mbaroni wasichana kwa kushiriki katika maandamano dhidi ya serikali nchini humo na kuitaja hatua hiyo kuwa ni ukandamizaji dhidi ya wapinzani.  

0 comments:

Post a Comment