Katika kile kinachotafsiriwa kuwa ni kusafisha idara zilizopo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko katika Idara ya Uhamiaji baada ya kumteua Johari Masoud Sururu kuwa Kamishna mpya wa Zanzibar.
Uteuzi huo wa Rais Kikwete umekuja siku moja tangu
alipomteua Kamishna wa Polisi, Hamdan Omari Makame kushika wadhifa huo
Zanzibar huku aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, Kamishna Mussa Ali
Mussa akiteuliwa kushika wadhifa mpya wa Kamishna wa Polisi Jamii.
Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga ilieleza kuwa kutokana na uteuzi
huo, aliyekuwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Mwinchumu Hassan Salim
atapangiwa kazi nyingine.
Kabla ya uteuzi huo ambao umeanza Novemba 24 mwaka huu, Sururu alikuwa Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania, Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Kabla ya uteuzi huo ambao umeanza Novemba 24 mwaka huu, Sururu alikuwa Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania, Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Agosti 28 mwaka huu baada ya kuongozana kwa
matukio ya watu kukamatwa na dawa za kulevya na meno ya tembo katika
viwanja vya ndege nchini, nje ya nchi na maeneo mbalimbali, Rais Kikwete
alifanya mabadiliko katika idara hiyo kwa kumteua Sylvester Mwakinyule
kuwa Kamishna Mkuu, Idara ya Uhamiaji.
Mwakinyule alichukua nafasi ya Magnus Ulungi
ambaye ilielezwa kuwa atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi huo,
Mwakinyule alikuwa Naibu Kamishna wa Uhamiaji na Mwambata wa Uhamiaji
katika Ubalozi wa Tanzania, London, Uingereza.
Katika uteuzi wa juzi, Rais Kikwete alifanya
mabadiliko katika idara nyingine ya wizara hiyo kwa kuwapandisha vyeo
maofisa waandamizi wanne wa Jeshi la Polisi, pamoja na kufanya uteuzi wa
nafasi za madaraka kutokana na mabadiliko ya muundo wa jeshi hilo.
Waliopandishwa vyeo ni pamoja na Isaya Mungulu ambaye anakuwa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Robert Manumba ambaye amestaafu.
Waliopandishwa vyeo ni pamoja na Isaya Mungulu ambaye anakuwa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Robert Manumba ambaye amestaafu.
Awali, Mungulu alikuwa Mkuu wa Ufuatiliaji na
Tathmini (CID) na baada ya Manumba kustaafu Novemba 11 mwaka huu,
aliteuliwa kukaimu nafasi hiyo.
Maofisa wengine waliopandishwa vyeo kuwa
Makamishna wa Polisi (CP) ni Ernest Mangu, Thobias Andengenye,
Abdulrahaman Kaniki na Makame.
Rais Kikwete pia amempandisha cheo Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Athuman Diwani kuwa Naibu Kamishna
wa Polisi na kumteua kuwa Naibu DCI.
Walioteuliwa katika nafasi za madaraka ni Clodwig
Mtweve (Kamishna wa Fedha na Utaratibu wa Ugavi na Usafirishaji wa Watu
na Vitu (Logistics), Paul Chagonja (Kamishna wa Operesheni na Mafunzo).
Mangu (Mkurugenzi wa Usalama wa Jinai), Andengenye (Kamishna wa Utawala na Utumishi) na Kaniki (Uchunguzi wa Ushahidi wa Jinai).
0 comments:
Post a Comment