WATOTO wa kike 100 wamelawitiwa na kubakwa katika manispaa ya Ilala,
Dar es Salaam, huku wanawake 20 nao wakifanyiwa vitendo hivyo kati ya
Aprili hadi Desemba mwaka huu.
Takwimu zinaonyesha kuwa watoto wa kiume 56 na wanaume 10 walilawitiwa
katika kipindi hicho huku waliopigwa wakiwa ni watoto 33 na watu wazima
16.
Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Dk. Willy Sangu, alitoa
takwimu hizo jijini Dar es Salaam jana katika uzinduzi wa kituo cha
‘One Stop’ katika Hospitali ya Amana ambacho kitakuwa kikitoa matibabu
kwa wahanga wa matukio ya ukatili wa kijinisia.
Dk. Sangu alisema katika matukio hayo watoto sita walitelekezwa na
watu watano walichomwa moto, vitendo ambavyo vinadaiwa kuongezeka kwa
kasi ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Hata hivyo, alisema pamoja na idadi hiyo ni mashauri matatu ndiyo
yamefikishwa mahakamani, hali inayochangiwa na watendewa kushindwa kutoa
ushirikiano.
Alizitaja sababu za ushirikiano mdogo ni wanaotenda vitendo hivyo kuwa
ndugu wa karibu wa wahanga hao na hivyo kuamua kumaliza kesi hizo
nyumbani.
Kutokana na hali hiyo, Dk. Sangu alisema kufunguliwa kwa kituo hicho
kutakuwa ni mkombozi kwa wahanga hao, kwani mpaka sasa ni watu 257
walioifishwa hospitalini hapo kwa kufanyiwa vitendo hivyo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Juma Bwire, alisema kufunguliwa
kwa kituo hicho ni mwendelezo wa Jeshi la Polisi katika kupinga ukatili
kwa kinamama na watoto.
Dec 6, 2013
Kasi Ya Kulawiti Watoto Yaongezeka
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment