Nov 9, 2013

Israel inakabiliwa na hatari ya kutengwa -John Kerry





Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani ametahadharisha juu ya kutengwa utawala wa Kizayuni wa Israel ulimwenguni. 

John Kerry ameutahadharisha utawala wa Israel kwamba, kama mazungumzo  ya amani baina ya Wazayuni  na Wapalestina hayataendelea, kuna hatari kwa utawala huo ghasibu kutengwa kimataifa. Kerry amesisitiza kuwa, bila shaka kama mazungumzo kati ya Wapalestina na Wazayuni hayatafikia kwenye natija, kampeni dhidi ya Israel zitapamba moto ulimwengu kote. Duru mpya ya mazungumzo ya amani ilianza tena mwezi Julai mwaka huu nchini Marekani, baada ya kukwama kwa takribani miaka mitatu kutokana na hatua za utawala wa Israel kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Mashariki mwa Baitul Muqaddas. Inafaa kuashiria hapa kuwa, wakati John Kerry anafanya safari katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, utawala wa Israel ulitangaza mpango mpya wa kujenga nyumba zaidi ya 1,800 katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Israel.

0 comments:

Post a Comment