MASJID AL AMIN ILIYOPO MANZESE UZURI.
Waislamu wamefanikiwa kuvunja sherehe za Shoga zilizokuwa zifanyike mwishoni mwa wiki iliyopita.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi ya Tarehe 5/10/2013 majira ya saa tatu usiku eneo la manzese uzuri,ambapo shoga huyo aliandaa sherehe za kutimiza miaka Ishirini na mbili ya Kuzaliwa kwake.
Akizungumza na munira blog,Katibu Mkuu wa Baraza la Wadhamini la Masjid Al amin Ustaadh Said Mpangalile alisema "tulipata taarifa kwamba kijana (Jina lake tunalihifadhi) ambaye tabia yake ya Ushoga ipo wazi hapo mtaani,anafanya sherehe za kuzaliwa na miongoni mwa aliowaalika ni mashoga wa Kinondoni na Mwananyamala".
"Kwa kuwa tunamfahamu tabia zake,tukakubaliana twende kwao tukapate uhakika,baada ya kufika kwao tukakuta kuna muziki mkubwa na baadhi ya mashoga wenzake wakiwepo"alisema.
Akieleza zaidi ustadh Said anasema,"tukafanikiwa kuonana na mama yake mlezi na kumwambia kwamba sisi viongozi wa dini hatuko tayari kuona sherehe hiyo inaendelea".
Ustaadhi Said aliendelea kusema kwamba yule mama alipinga kwa madai wao wana kibali na shughuli yao ni halali.
"Kwa busara tukawasiliana kwa njia ya simu na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Manzese Uzur Mhe Johnas Halimoja ambaye kwa wakati huo alikuwa maeneo ya mbali".
"Wakati tunaendelea kuwasiliana na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa mara likajiri tukio la kumletea keki Shoga huyo,keki hiyo ililetwa na msichana aliyevaa nusu uchi kwa asilimia thamanini na tano"alisema kwa masikitiko..
"Ndugu mwandishi hali hiyo tulishindwa kuivumilia yule binti tulimvuta na tukaimwaga keki na vurugu ikaanza hadi walipokuja polisi na kubaini kwamba sherehe hiyo haikuwa na kibali hatimaye kuwaamuru wavunje sherehe,unafikiri tukio lile lingeendelea lingetoa funzo gani hasa kwa watoto"mwisho wa kumnukuu.
USTAADH SAID MPANGILILE,KATIBU MKUU BARAZA LA WADHAMINI MASJID AL AMIN,MANZESE UZURI,DAR ES SALAAM.
Jana usiku munira blog ilifika ofisini kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Manzese Uzuri ambapo alikiri kutokea tukio hilo.
"Kwa kweli nalifahamu tukio hilo,japo ni ngumu kuthibisha zinaa,lakini Kijana huyo anajulikana kuwa ni mtoto mchafu tangu akiwa shule ya msingi hadi sasa".alisema.
"Mwenyekiti huyo alikana ofisi yake kutoa kibali cha sherehe hiyo na kudai kwamba sherehe hizo hazihitaji kibali zaidi ya wao kuwajibika kusimamia ulinzi kwa shughuli zote za kijamii"
Leo asubuhi munira blog ilifika Polisi Magomeni lakini mkuu wa polisi kituo cha magomeni amesema halijuwi tukio hilo.
JOHNAS HALIMOJA,MWENYEKITI SERIKALI YA MTAA MANZESE UZURI.
0 comments:
Post a Comment