KATIKA KUUKARIBISHA MWEZI WA
RAMADHANI,WAISLAMU WASHAURIWA
TUKIMBILIE FURSA
ZINAZOPATIKANA KATIKA MWEZI WA RAMADHAN.
- TUMFANYE SHAITWANI KUWA NI ADUI YETU.
- TUSIPOTEZE MUDA KWA MAMBO YASIYOFAA.
Na mwandishi wetu
wa munirablog.
Waislamu wametakiwa
kuzichangamkia na kuzitumia kikamilifu fursa zinazopatikana katika Mwezi
Mtukufu wa Ramadhan ambao unatarajiwa kuanza wiki ijayo Inshaa Allah.
Hayo yamesemwa na
Sheikh Ramadhan Khamis Kwangaya kutoka Taasisi ya HAY-ATUL ULAMAA yenye makao
yake Jijini Dar es salaam.
Ameyasema hayo
usiku huu wakati akitoa mada ya Fursa na Changamoto zilizopo ndani ya Mwezi wa
Ramadhan ikiwa ni muendelezo wa mihadhara ya kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
inayoandaliwa na kamati ya mihadhara ya Masjid Qiblatain.
Akiwahutubia Waislamu
wa Masjid Tawwab wa Magomeni Makuti Manispaa ya Kinondoni Jijini
Dar es salaam,Sheikh Kwangaya alisema uwepo wa mwezi wa Ramadhan
ni Fursa pekee kwa muislamu kuitumia vizuri Ofa nono aliyoiweka MwenyeeziMungu
kwetu.
“Kwa siku tunafunga masaa
yasiyozidi 14,utakapoifunga vizuri fahamu utalipwa thawabu kwa kila sekunde
moja,na thawabu katika mwezi wa Ramadhan zinazidishwa hadi kufikia mara sabini
(70) sasa malipo haya unayapata hapa duniani huku faida ya malipo haya
utayakuta Akhera kwa wewe kuwekwa mbali na moto wa Jahannamu kwa zaidi ya miaka
1,500,000”.
Aliwatanabaisha
waislamu kwamba Thawabu hizi atazipata yule aliyefunga kikamilifu kwa maana
kufunga tumbo lake
na viungo vyake huku
akisema kufunga kinyume cha hivyo ni khasara kwa mfungaji huku akinukuu maneno
ya Mtume s,a,w aliposema yawezekana mfungaji asiambulie chochote zaidi ya
kushinda njaa na kiu.
Alisema tukizitumia
vizuri fursa hizi ndani ya mwezi wa Ramadhan hatutokuwa na sababu za kukosa
Radhi za Mwenyeezi Mungu.
Aidha aliwaasa
waislamu kuzikabili changamoto zinazopatikana ndani ya mwezi wa Ramadhan kwa
kuanza sasa kumfanya Sheitwani kuwa ni adui yetu.
“Ndugu
zangu waislamu tufahamu ya kwamba Mtume s,a,w aliposema ya kwamba Funga ni
kinga,Shaitwani alilifahamu neon hili vizuri sana,ndipo akaweka mipango
mikakati dhidi ya waislamu,mipango hii ameigawa sehemu mbili,sehemu ya kwanza
ni kumshawishi na kumlaghai muislamu afanye maasi sana kabla ya kufunga na
sehemu ya pili ni kumshawishi na kumlaghai muislamu afanye maasi siku za mwanzo
tu baada ya kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani”,mwisho wa
kumnukuu.
Aliendelea kusema,”hakuna
mwezi ambao baadhi ya waislamu wanafanya maasi sana kama katika mwezi huu wa
shaaban hasa katika siku za mwisho wa shaaban,na mwanzoni mwa mwa mfungo mosi,ndiyo maana kila kona utasikia
kwamba kuna vunja jungu wakimaanisha kufanya maasi ya mwisho mwisho kabla ya
kuanza kwa mfungo wa Ramadhan,shaitwani kawapambia haya kwa kuwa anajuwa fika
kwamba ukianza Mwezi wa Ramadhan yeye anafungwa minyororo.”alisema.
Huku waumini wa
kiislamu wakiendelea kumsikiliza,Shekh Kwangaya alisema,ukiingia katika ibada
ya swaumu hali ya kuwa tayari umeshajipakatisha madhambi una athirika kifikra
na kiimani na uwezo wa kufanya ibada kwa umakini unakosekana,sasa hapa
shaitwani atakuwa kafanikiwa lengo lake.
Aidha
aliwafahamisha waislamu ya kwamba mpango mkakati wa pili wa shaitwani dhidi ya
waislamu ni kumfanya muislamu amuasi Mungu mara tu baada ya kumalizika kwa
mfungo wa Ramadhani ili aiharibu funga yake yote ya mwezi mzima.
Aliwakumbusha
waislamu kwamba lengo la kufunga ni kumfanya mtu afikie daraja la Ucha Mungu na
maana ya Ucha Mungu ni mtu kujitenga na
kujiepusha na maasi yote.
Aliwashauri waislamu
kufanya wingi wa Swala za usiku,Swala za kablia na baadia,kusoma Qur aan,kuleta
adhkaar,kuwahi msikitini kwa lengo la kuisubiri Swala,na kukaa msikitini baada
ya swala,matendo haya yanafaida kubwa sana kwetu hasa ndani msimu wa mwezi wa Ramadhan.
Kamati ya
maandalizi ya mihadhara ya Masjid Qiblatain chini ya uenyekiti wa Sheikh Ally Bassaleh
imekuwa na desturi ya kuandaa mihadhara ya aina hii kwa kila mwaka na kuwapa
faida nyingi waislamu,ambapo kesho mhadhara utakuwa katika Msikti wa Mtoro na
mhadhiri atakuwa Sheikh Nurdin Kishki,Inshaa Allah blog ya munira itakuwepo na itawahabarisha.
0 comments:
Post a Comment