Wakati Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec), ikitangaza ratiba ya Uchaguzi Mkuu, wanasiasa wenye asili ya Pemba wameamua kudhibiti nafasi ya urais Zanzibar baada wagombea watano kutoka kisiwani humo kutajwa kuwa na mipango wa kugombea, akiwamo Rais Dk Ali Mohamed Shein .
Kama wanasiasa hao watasimama kwenye dhamira hiyo
na mmoja kuibuka mshindi, kisiwa hicho kitaandika historia mpya ya kutoa
Rais katika vipindi viwili tangu uhuru wa Zanzibar mwaka 1964.
Marais waliowahi kushika wadhifa huo kupitia Chama
cha Afro Shiraz Part (ASP), kabla ya kuungana na Tanu mwaka 1977 na
kuzaliwa CCM, ni Rais wa kwanza Sheikh Abeid Amani Karume, Aboud Jumbe
Mwinyi, Idrisa Abdulwakili, Dk Salmin Amour Juma na Amani Abeid Karume.
Wagombea waliotangaza nia hadi sasa ni Makamu
Mwenyekiti NCCR Mageuzi, Ambari Khamis Haji, Katibu Mkuu wa Tadea, Juma
Ali Khatibu, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Hamad Rashid
Mohamed (ADC) na Dk Ali Mohamed Shein anayetajwa kutaka kuendelea na
wadhifa huo.
Mchuano mkali unatarajiwa kuonekana kati ya
Mgombea wa CCM, Dk Shein na Maalim Seif wa CUF kutokana na vyama vyao
kuwa na ushindani mkubwa kisiasa tangu.
Uchaguzi wa mwaka 2010, Dk Shein alishinda kwa
asilimia 51, huku Maalim Seif akipata asilimia 49 na kulazimika kuunda
Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
0 comments:
Post a Comment