Meja Jenerali Muhammad Ali Jafari, Kamanda Mkuu wa Jeshi la
Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, barua ya Kiongozi
Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Ulaya na Amerika
Kaskazini ni marhala na hatua mpya ya kuyatangaza Mapinduzi ya Kiislamu.
Meja Jenerali Ali Jafari amesisitiza kuwa, barua ya Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei imeingiza kazi ya kuyatangaza Mapinduzi ya Kiislamu katika hatua mpya.
Akihutubia wajumbe wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na Kusimamia Kazi Zake, Meja Jenerali Muhammad Ali Jafari, amesema Mapinduzi ya Kiislamu yamekuwa yakipiga hatua kwa kasi na mfano wa wazi ni hii barua ya Ayatullah Khamenei kwa vijana wa Ulaya na Amerika Kaskazini.
Ikumbukwe kuwa, Januari 21 mwaka huu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alitoa ujumbe wa kihistoria kwa vijana wa Ulaya na Amerika Kaskazini.
Sehemu moja ya ujumbe huo inasema: “Ninachopenda kukuombeni ni kwamba msiruhusu njama za kuoneshwa sura mbaya na ovu kuhusiana na Uislamu kuwa kizuizi katika hisia zenu na kukuzuieni kuhukumu mambo kiuadilifu. Leo hii zana za kisasa za mawasiliano zimevunja mipaka ya kijiografia, hivyo msiruhusu wakufungeni ndani ya mipaka ya kupandikizwa na isiyo na ukweli.
Ijapokuwa mtu mmoja hawezi kuziba mapengo yote yaliyopandikizwa kwa muda mrefu sasa, lakini kila mmoja wenu anaweza kujenga daraja la fikra na insafu kwenye mapengo hayo kwa lengo la kujielimisha yeye mwenyewe mambo sahihi na vilevile kuwaelimisha watu wanaomzunguka.”

0 comments:
Post a Comment