Abd Rabbu Mansour Hadi, Rais
aliyejiuzulu nchini Yemen ametoroka kutoka mji mkuu Sana'a na kukimbilia
katika mji wa bandari wa Aden baada ya kuwa chini ya kifungo cha
nyumbani kwa majuma kadhaa.
Watu wa karibu naye wanasema Hadi ametoroka
kutoka nyumbani kwake alikokuwa akizuiliwa na wapiganaji wa harakati ya
Ansarullah na ameelekea katika mji wa Aden ulioko kusini mwa Yemen.
Januari 22, Hadi alitangaza kujiuzulu
pamoja na serikali ya Waziri Mkuu, Khalid Bahah baada ya kushitadi
mgogoro nchini humo.
Wachambuzi wengi wanasema rais wa zamani wa Yemen
ameamua kukimbilia mjini Aden kwa kuwa ndiko anakoungwa mkono zaidi na
wazee wa kikabila wa mji huo.
Baadhi ya duru zinaarifu kuwa, kiongozi
huyo aliyejiuzulu anapanga kwenda Saudi Arabia au Marekani kutokana na
kuendelea kudhoofu afya yake.
0 comments:
Post a Comment