Habari kutoka Misri zinasema kuwa, wanafunzi 5 wa Chuo Kikuu cha al-Azhar watatakiwa kufika mbele ya Mahakama ya Kijeshi baada ya mafaili yao kuhamishwa kwenye mahakama hiyo.
Jana Jumapili, mahakama moja ya kiraia iliamua kupeleka mafaili ya wanafunzi hao kwenye mahakama ya kijeshi ikidai kwamba haina mamlaka ya kusikiliza kesi za ugaidi na uharibifu wa mali ya umma.
Wanafunzi hao walikamatwa mwezi Januari mwaka huu wakati walipokuwa wakiandamana kupinga hatua ya jeshi ya kumpindua Mohammad Mursi, rais wa kwanza kuchaguliwa kihalali na wananchi.
Mashirika ya kijamii yamelalamikia hatua hiyo huku yakisema Misri imerudi tena katika 'siku za giza' ambapo serikali ilikuwa ikiendeshwa kijeshi
Mwezi uliopita, Rais Abdul Fattah al-Sisi aliidhinisha sheria inayoruhusu raia wa kawaida kushtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi.
0 comments:
Post a Comment