Waliobakwa na kisha kuozwa
waume katika wilaya ya Wete mkoa wa kaskazini Pemba, wamesema ndoa za mkeka
zinazofungwa kama sulhu, zinachangia kwa kiasi kikubwa kasi ubakaji katika
jamii.
Uchunguzi uliofanywa na
mwandishi wa habari hizi, umeonesha jamii imekuwa na uharaka wa kuwafungisha
ndoa mara wanapobaini kuwepo vitendo hivyo,wakidhani ndio sulhu ya kuvitokomeza
badala yake vimekuwa vikichangia kuongezeka.
Uchunguzi umebaini imekuwa na
kawaida kuharakia sulhu ya ndoa, hata kama shauri hilo limeshafikishwa katika
vyombo vya sheria, jambo ambalo huwapa jeuri na kiburi wabakaji.
Mmoja kati ya waathirika wa
ubakaji na kisha kuolewa mwenye miaka 17, mkaazi wa shehia ya Mchangamdogo
wilayani humo, alisema binafsi baada ya kujihisi ameshapewa ujauzito,
alikimbilia kituo cha polisi na kisha muhusika kukamatwa.
Awali, alimueleza mpenzi wake
huyo kwamba, ameshampa ujauzito na alipokataa, ndipo alichukua uamuzi wa
kukimbilia kituo cha polisi Wete,inagwa kesi hiyo haikufikishwa mahakamani.
0 comments:
Post a Comment