Kundi la watetezi wa haki za
binadamu wa Yemen na waandishi wa habari wamegundua njia za chini kwa
chini na seli za wafungwa zilizo kinyume cha sheria huko San'aa mji mkuu
wa nchi hiyo.
Seli na njia hizo za chini ya ardhi zimegunduliwa ndani
ya kituo cha kijeshi ambacho kilikuwa kikisimamiwa na Meja Jenerali
mtoro Ali Mohsen al Ahmar, kaka wa kambo wa dikteta wa zamani wa Yemen
Ali Abdullah Saleh.
Abdurahman Abdul-wahid, afisa wa kituo
cha haki za raia cha Yemen amesema kuwa seli hizo walizozikuta chini ya
ardhi zipo katika hali ya kutisha na kwamba wamepata pia baadhi ya
minyororo ambayo ilikuwa ikitumika kutesea watu.
Itakumbukwa kuwa
wapiganaji wa harakati ya Ansarullah walikidhibiti kituo hicho cha
kijeshi baada ya kujiri mapigano makali huko San'aa kati yao na vikosi
vitiifu kwa Meja Jenerali mtoro Ali Mohsen al Ahmar.
0 comments:
Post a Comment