Spika wa Majlisi ya Ushauri ya
Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, mashambulizi ya Marekani dhidi ya
kundi la Daesh ni kisingizio tu cha kuangamiza miundombinu ya Syria.
Shirika la Habari la Fars limemnukuu Dk Ali Larijani akisema hayo leo
wakati wa kufunga Maonyesho ya Tano ya Kitaifa ya Vitabu vya Kujihami
Kutakatifu hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa, Rais wa Marekani amedai
kuwa ataliangamiza kabisa kundi la Daesh lakini ukweli wa mambo ni kuwa
hayo ni madai tu yasiyo na ukweli, kwa uhakika wa mambo ni kwamba lengo
la Marekani ni kuangamiza miundombinu ya Syria. Spika wa Bunge la Iran
vile vile amewaambia viongozi wa nchi zinazoshirikiana na Marekani
kwamba, lengo la Marekani ni kuzidi kuwa na ushawishi wa kijeshi nchini
Iraq na kuwaweka madarakani vibaraka wake nchini Syria.
Dk Larijani
ameongeza kuwa, hatua ya Iran ya kujihami kiume katika vita vya miaka
minane vilivyoanzishwa na utawala wa wakati huo wa Iraq imeathiri moja
kwa moja matukio mengine katika eneo hili yakiwemo ya vita vya siku 33
na 22 vya Lebanon na Ghaza, na inabidi matukio ya wakati wa vita vya
kujihami kutakatifu Iran yachunguzwe zaidi ili kuzidi kupata uzoefu wa
kujilinda.
0 comments:
Post a Comment