Oct 1, 2014

Marais wanne ni miongoni mwa Mahujaji mwaka huu

hujaj
Mahujaji Makkah

Marais wanne ni miongoni mwa mamilioni ya Waislamu wanaotekeleza ibada ya Hijja katika mji mtukufu Wa Makka nchini Saudi Arabia.


Marais hao ni Omar Sheikh Wa Somalia, Omar al-Bashir Wa Sudan, Abdullahi Yameen Wa Maldives na Abdul Hamid Wa Bangladesh.

Ibada ya Hijja ni nguzo ya 5 katika dini ya Kiislamu, iliyifaradhishwa kwa waumini walio na nafasi nzuri ya kifedha.

Ibada hiyo huandamana na funga ya Arafa ambayo ni tarehe 9 ya mwezi Wa Dhulhijja, na kufuatia na sherehe za Iddul-Adh’ha, tarehe 10 ya mwezi huo katika kalenda ya Kiislamu.

0 comments:

Post a Comment