WAZIRI wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)
Mansour Yussuf Himid anayekabiliwa na kesi ya kupatikana na silaha ya
moto na risasi 407 amewasilisha maombi matatu mahakamani ikiwemo
kuruhusiwa kusafiri nje ya nchi kuanzia Oktoba 22 mwaka huu,
imefahamika Visiwani humo jana.
Maombi hayo yamewasilishwa na Wakili wake Samah Salaha mbele ya Hakimu
wa Mahkama ya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Khamis Ramadhan Abdalla, akitaka mteja wake hapatiwe ruhusa ya kwenda kufanyiwa uchunguzi wa
afya yake nchini India pamoja na kufanyiwa mazoezi ya viungo vya magoti
nchini Ujerumani.
Samah alisema kwamba Mansour amekuwa akifanyiwa uchunguzi wa afya yake
kila mwaka nchini India na kuomba mahakama kuondoa mashariti ya dhamana
yake ya kutosafiri nje ya nchi kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Abraham
Mwampashi Agositi m18 mwaka huu.
:Naomba kuwasilisha maombi ya mteja wangu anataka kusafiri nje ya nchi
kuanzia Oktoba 22 hadi Novemba 12 nchini India na Ujerumani kuchunguza
afya yake na kufanya mazoezi ya viungo vya magoti nchini
Ujerumani:alisema Samah.
Alisema kutokana na mazingira hayo pia mteja wake apewe hati ya
kusafiria pamoja na kuruhusiwa kusafiri kati ya Zanzibar na Dar es
salaam kutokana na shughuli zake za kibiashara na kifamilia.
Mwanasheria huyo alisema kwakuwa Mama yake Masour baadhi ya wakati
analazimika kufuata matibabu Tanzania bara vizuri mteja wake akapunguziwa mashariti ili hapate nafasi ya kumuhudumia mama yake hasa
kwa kuzingati yeye ndiyo Mtoto mkubwa wa Kiume katika familia yao.
Hata hivyo Mwendesha mashtaka wa Serikali Ally Yussuf Mohamed alisema
kwamba upande wa mashtaka hauna pingamizi kama mshtakiwa hataweza
kuwasilisha nyaraka za kuthibitisha kama amekuwa akitibiwa nje ya nchi
kila mwaka kwa kuwasilisha nyaraka pamoja na nyaraka za biashara anazofanya kati ya Zanzibar na Tanzania bara.
Upande wake Hakimu Khamis Rmadhani Abdalla, alimtaka mshtakiwa
kuwasilisha nyaraka hizo zikiwa katika mpangilio wa kisheria pamoja na
maombi yake
Waziri huyo wa zamani amefunguliwa mashtaka baada ya kupekuliwa nyumbani
kwake Chukwani Zanzibar na kukamatwa na silaha ya moto aina ya bastola
na risasi 407 kinyume na sheria na yupo nje kwa dhamana ya mashariti ya
kutosafiri bila ya ruhusa ya mahakama, fedha taslimu Milioni tatu,
wadhamini wawili wenye bondi ya shilingi milioni tano kila mmoja na hati
ya kusafiria kushikiliwa na Mahakama
Kuhusu kesi ya msingi Mwansheria wa SMZ Ally Yussuf Mohamed alisema
kwamba upelelezi wake bado kukamilika lakini kwa mujibu wa sheria ndani
ya miezi tisa utakuwa umekamilika na kutoa nafasi kesi kuanza
kusikilizwa kabla ya kutolewa hukumu.
0 comments:
Post a Comment