Oct 1, 2014

BREAKING NEWS-BUNGE LAKANUSHA KUKAMATWA MWANASHERIA MKUU ZNZ

Hatimae Idara ya Habari Ofisi ya Bunge Maalum la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekanusha juu ya tetesi zilizozagaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii kwamba Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar amekamatwa.

 

Hali hiyo ilitokana na hatua ya Mhe Othman Masoud Othman ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupiga kura ya hapana kwa baadhi ya ibara ya rasimu ya katiba hali iliyopelekea hali ya hewa ukumbini hapo kuchafuka.


Kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa Bungeni hapo kulikoambatana na zomea zomea askari wa bunge walimsindikiza hadi katika gari yake ili asibughudhiwe hali ilitafsiriwa na baadhi ya watu kwamba amekamatwa,ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

0 comments:

Post a Comment