Sep 2, 2014

PLO yataka Palestina kujiunga na mahakama ya ICC

Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) imemtaka Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kufanya jitihada za Palestina kuwa mwanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ili Israel iweze kushitakiwa.

 
Tisair Khalid afisa mtendaji wa PLO amesema kuwa, ili kuhukumiwa viongozi wa utawala wa kizayuni wa Israel Palestina inalazimika kutia saini makubaliano ya mahakama ya ICC na kuwa mwanachama wa korti hiyo ya kimataifa.

 Ameongeza kuwa, miongoni mwa jinai zinazoikabili Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni kughusubu ardhi za Wapalestina kwa ajili ya kujenga vitongoji vya walowezi. 

Ameeleza kuwa, kwa mujibu wa mada  nambari 8 ya mkataba wa mahakama ya ICC, ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina unahesabiwa kuwa ni jinai ya vita, hivyo unapaswa kusitishwa.

Licha ya Israel kuwashambulia na kuwaua raia wa Palestina bila hatia, utawala huo ghasibu pia umekuwa ukipora ardhi za Wapalestina na kuwalazimisha wakazi wake kuwa wakimbizi.

0 comments:

Post a Comment