Sep 2, 2014

Book Haram yaua Wakristo nchini Nigeria

Kundi la kigaidi la Boko Haram nchini Nigeria limewaua kwa kuwakata vichwa wafuasi wa dini ya Kikristo, jinai ambayo inashabihiana na zile zinazofanywa na kundi la kitakfiri la Daesh nchini Iraq na Syria.

Mashuhuda wanaeleza kuwa, wanachama wa kundi hilo ambalo limeshadidisha mauaji na jinai katika miezi ya hivi karibuni nchini Nigeria, wamekuwa wakiwatia hofu raia wa maeneo wanayoyadhibiti kwa kuwachinja watu kama mbuzi na kuwamiminia risasi ovyo. 

Inaelezwa kuwa, wanamgambo wa kundi hilo wamefanya mauaji hayo katika mji wa Madagali, kaskazini mashariki mwa Nigeria, mji ambao hivi karibuni ulidhibitiwa na Boko Haram. 

Jason Obasuyi, mmoja wa makasisi wa mji huo amenukuliwa akisema kuwa, baada ya wanachama wa kundi hilo kuudhibiti mji wa Madagali, walianza kuwachinja Wakristo wakiwamo viongozi wa kanisa. 

Hali hiyo imeshuhudiwa pia katika miji ya Gamboru na Ngala iliyopo katika mpaka wa Cameroon na Nigeria ambayo ilidhibitiwa na wanachama wa kundi hilo siku ya Alkhamis iliyopita.

0 comments:

Post a Comment