Sep 2, 2014

Mji wa Tripoli wadhibitiwa wanamgambo wa Fajr

Mji wa Tripoli wadhibitiwa wanamgambo wa Fajr




Hali ya mchafukoge inaendelea kushuhudiwa nchini Libya ambako imeriporiwa kuwa mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli sasa umeangukia mikononi mwa kundi la wanamgambo la Fajru Libya.
Hayo yamejiri huku mapigano yakiendelea kwa wiki kadhaa sasa kati ya makundi hasimu kwenye mji huo. 

Serikali ya mpito ya Libya imetangaza kuwa, wanamgambo wenye silaha wanakalia majengo mengi ya serikali katika mji mkuu na kwa sababu hiyo serikali itahamishia shughuli zake katika miji mingine hadi pale usalama utakapoimarishwa. 

Katika mji wa mashariki mwa Libya wa Benghazi pia  mapigano yanaendelea kati ya vikosi wanajeshi watiifu kwa jenerali mstaafu Khalifa Haftar na kundi la kisalafi la Ansar al Sharia.

 Hayo yanajiri huku Waziri Mkuu mpya wa Libya akitarajiwa kutangaza serikali yake mpya hapo kesho.

0 comments:

Post a Comment