Aug 3, 2014

Israel yabomboa misikiti na mahospitali Ghaza

Utawala wa Kizayuni wa Israel haujatosheka kwa kuwaua kwa umati wanawake na watoto wa Ghaza bali pia umeharibu kwa mabomu idadi kubwa ya misikiti na mahospitali katika ardhi hiyo ya Wapalestina.

Kanali ya Televisheni ya Al Mayadeen imeripoti kuwa katika hujuma ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza mahospitali na vituo vya afya 44 vimeharibiwa kabisa. 

Hivi sasa aghalabu ya Wapalestina waliojeruihiwa katika vita vya Ghaza hawana sehemu za kupata matibabu.  

Mbali na kubomoa mahospitali, jeshi la Kizayuni pia limeharibu kabisa misikiti 41 katika Ukanda wa Ghaza. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jeshi la utawala haramu wa Israel limeshambulia na kubomoa misikiti hiyo ambayo ilikuwa sehemu ya hifadhi ya Wapalestina ambao nyumba  zao zimeharibiwa kwa mabomu.

Wakati huo huo katika kujibu jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel, Brigedi ya Izzuddin Qassam tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imevurumisha makombora katika miji inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Aidha wanamapambano ya Palestina wamefanikiwa kuwaangamiza wanajeshi wasipungua 131 wa utawala wa Kizayuni katika vita vya Ghaza.

0 comments:

Post a Comment