Aug 1, 2014

Mashahidi wafikia 1450, majeruhi 8270 huko Ghaza

Idadi ya wahanga wa mashambulizi ya siku 25 mtawalia ya utawala katili wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza, imefikia 1450, na zaidi ya watu wengine 8270 wamejeruhiwa. 

Habari zinasema kuwa, jeshi la utawala katili wa Kizayuni limeendelea kuyashambulia maeneo ya Abasan, mashariki mwa mji wa Khan Yunus na kuwaua shahidi watu kadhaa huku wengine wakiuawa na mashambulizi ya ndege za utawala huo katika eneo la Rafah.
Aidha habari zinasema kuwa, vifaru vya jeshi la Israel vimeendelea kushambulia maeneo ya mashariki mwa Ghaza usiku mzima uliopita na hivyo kuifanya idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi kuongezeka sana. 

Kwengineko Wizara ya Afya katika ukanda huo imetangaza kuwa, imekuwa vigumu sana kwa magari ya wagonjwa kufika katika maeneo yote kutokana na uchache wa magari na vifaa vya tiba na kwamba, kuna tishio la kuongezeka mno wahanga wa jinai hizo za Wazayuni. 

Awali waandishi wawili wa habari mmoja wa kanali ya al-Aqsa, Samih al-Iryan na mwengine wa mtandao mmoja wa habari, Rami Rayyani, na madaktari wawili waliuawa shahidi siku ya Jumatano katika jinai ya Israel iliyofanywa katika soko la eneo la Shujaiya huko Ghaza, ambapo makumi ya raia wengine waliuawa wakati walipokuwa wamekwenda kununua huduma muhimu za chakula.

0 comments:

Post a Comment