Jul 30, 2014

Takwimu za HRW kuhusu maafa ya Ghaza (kichanga chafariki)



Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limetangaza tena kuwa asilimia 82 ya Wapalestina waliouawa katika mashambulizi ya kinyama ya Israel katika Ukanda wa Ghaza ni raia wa kawaida.


Taarifa ya HRW imesema kuwa jeshi la Israel limezidisha mashambulizi yake dhidi ya raia wa Ghaza katika siku za hivi karibuni na kwamba limeua watu wote wa familia zipatazo 56 katika mashambulizi ya sasa kwenye eneo hilo. 


Shirika hilo limesisitiza kuwa Jeshi la Israel linalenga nyumba za raia wa kawaida na kwamba hicho ni kielelezo cha jinai za kivita.


Hadi sasa Wapalestina wasiopungua 1260 wameawa katika mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na jeshi la utawala katili wa Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Ghaza na maelfu ya wengine wamejeruhiwa.


Wakati huo huo kichanga kilichotolewa kwenye tumbo la mama mmoja wa Kipalestina aliyekuwa ameuawa na jeshi Israel, kimefariki dunia. 


Kichanga hicho kilitolewa kwenye tumbo la mama maiti, Shayma al-Sheikh Qanan, aliyeuawa katika shambulizi la Israel Jumamosi iliyopita na kuwekwa kwenye vyombo maalumu kutokana na kuwa kilikuwa bado hakijakamilisha miezi tisa ya kuzaliwa.

0 comments:

Post a Comment