Jul 30, 2014

Wapalestina wapenya kishujaa na kumaliza Wazayuni



Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imetoa mkanda wa video unaowaoonyesha wanamamapambano wake wakiwaangamiza wanajeshi kadhaa wa Israel katika shambulizi walilolifanya katika mnara wa doria ya kuchunga moto karibu na eneo la Ukanda wa Ghaza.
Mkanda huo wa video uliotolewa jana jioni na harakati ya Hamas unaonyesha picha ya wanajeshi kadhaa wa Israel walioangamizwa na wanamapambano wa Kiislamu hapo juzi.


Makomandoo wa Hamas walitumia njia za chini kwa chini karibu na mpaka wa Ghaza kuushambulia mnara huo wa doria huko Nahal Oz na kufanikiwa kuwaangamiza wanajeshi watano wa Israel. 


Duru za habari za Israel zimetangaza kuwa hadi sasa wanajeshi 130 wa Israel wamelazwa hospitalini, kumi wakiwa katika hali mahututi. 

Utawala wa Kizayuni umethibitisha kuangamizwa wanajeshi wake 53 huku harakati ya Hamas ikisema kuwa wanajeshi wa Israel walioangamizwa hadi sasa ni zaidi ya 100. 

Hamas imeongeza kuwa, hiyo ni idadi ya wanajeshi wa Israel walioweza kuhesabiwa na wanamapambano wake na kwamba idadi ya wanajeshi wa Israel walioangamizwa ni zaidi ya hiyo.

0 comments:

Post a Comment