Jul 31, 2014

Misri yazuia misaada ya Iran kufika Ghaza

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeilalamikia Misri kwa kutotoa kibali kwa ndege za Iran zenye misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Wapalestina wanaokabiliwa na hujuma za Wazayuni katika Ukanda wa Ghaza. 

 Hussein-Amir Abdullahian Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema ni jambo lisilokubalika kwa Misri kuzuia misaada ya Iran inayojumuisha dawa na chakula kwa ajili ya watu wanaodhulumiwa huko Ghaza.
Abdullahian ametoa wito kwa wahusika nchini Misri kuchukua hatua za haraka za kutoa kibali kwa ndege za Iran ziingie nchini humo ili misaada hiyo iwafikie Wapalestina haraka iwezekanavyo. 

Ameongeza kuwa hivi sasa kuna idadi kubwa ya majeruhi wa Ghaza wakiwemo watoto na wanawake ambao wanasubiri ndege hizo za Iran ili waweze kusafirishwa kwa ajili ya kupataka matibabu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameelezea matumaini yake kuwa Misri itatekeleza wajibu wake wa kibinadamu, Kiislamu, kihistoria, na Kiarabu katika kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ghaza kwa kufungua kivuko cha mpakani cha Rafah haraka iwezekanavyo ili kurahisisha upelekwaji misaada katika eneo hilo. 

Ikumbukwe kuwa Misri ndio nchi pekee ya Kiarabu yenye mpaka wa pamoja na Ukanda wa Ghaza. Hata hivyo watawala wa Misri wamekataa kufungua mpaka huo. 

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif ametoa wito kwa nchi za Kiislamu kuanzisha kampeni ya kupelekea misaada ya dharura katika Ukanda wa Ghaza.

 Ameyasema hayo katika mazungumzo ya simu na mwenzaji wa Malyasia Dato Seri Anifah Aman.

0 comments:

Post a Comment