Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, ripoti za awali za wachunguzi
wa umoja huo, zinaonyesha kuwa mnamo tarehe 29 mwezi Machi mjini Bangui,
Jamhuri ya Afrika ya Kati, askari wa Chadi waliwashambulia raia wasio
na hatia na bila ya sababu yoyote kufanya hivyo.
Hayo yamesemwa na Rupert Colville, Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi mbele ya waandishi wa habari na kuongeza kuwa, msafara wa wanajeshi hao wa Chad uliwashambulia raia katika eneo la kibiashara la PK 12.
Ameongeza kuwa, baada ya shambulio hilo wananchi walikimbia ovyo kwa kuhofia usalama wao, huku askari hao wakiendelea kumimina risasi.
Hata hivyo Colville hakuelezea ni upande gani ulioanzisha mashambulizi hayo.
Ripoti za awali zinaonyesha kuwa, watu 30 waliuawa katika shambulio hilo huku watu wasiopungua 300 wakiwemo watoto, vilema, wanawake wajawazito na wazee, wakijeruhiwa.
Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa, wanajeshi hao wa Chad waliotekeleza shambulizi hilo, hawakuwa miongoni mwa wanajeshi wa Chad walio katika kikosi cha askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

0 comments:
Post a Comment