Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani anayeshughulikia masuala ya
usalama nchini Tunisia ameonya kutokana na hatari na vitendo vya
uharibifu vya kundi la Kisalafi la 'Answaru Sharia' kwa nchi hiyo na
nchi nyingine jirani.
Ridha Sifr amesisitiza kuwa, kundi la Answaru Sharia ambalo linajiarifisha kuwa na mafungamano na kundi la kigaidi la al-Qaida, limejiandaa kutekeleza uharibifu nchini Tunisia na nchi nyingine jirani.
Amesema kuwa, moja ya matatizo makubwa yanayoikabili nchi yake hivi sasa ni kupakana Tunisia na nchi zenye machafuko kama Libya ambako makundi mengi yenye kufurutu ada yanaendesha harakati zao na kuingia baadhi ya wanachama hao nchini Tunisia.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani anayeshughulikia masuala ya usalama nchini Tunisia, amekiri kwamba serikali imeshindwa kurejesha misikiti iliyoporwa na wanachama wa kundi hilo na kusisitiza kuwa, hadi sasa misikiti 150 katika maeneo tofauti ya nchi hiyo, haipo chini ya udhibiti wa serikali suala ambalo ni hatari sana kwa taifa.
Itakumbukwa kuwa tarehe 27 mwezi Agosti mwaka jana, serikali ya Tunis ililitangaza kundi hilo kuwa la kigaidi na kwamba ndilo lililotekeleza mauaji dhidi ya wanasiasa wawili wa nchi hiyo ambao ni Chokri Belaid na Mohammad Al Barahimi.

0 comments:
Post a Comment