Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea
Haki za Binadamu la Human Rights Watch ameeleza kuwa hakuna uadilifu
wowote wanaotendewa Waislamu katika nchi iliyokumbwa na mgogoro ya
Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Philippe Bolopin, Mkurugenzi wa Human Rights
Watch ameyasema hayo baada ya kurejea kutoka nchini humo.
Bolopin
amesema kuwa, wiki iliyopita aliwaonyesha maafisa wa ngazi ya juu wa
Jamhuri ya Afrika ya Kati, picha zilizokuzwa za mwanaume mmoja wa
Kiislamu aliyekuwa akichomwa kisu na askari jeshi hadi kuuliwa huko
Bangui mji mkuu wa nchi hiyo na kuwauliza ni hatua zipi zinachukuliwa
ili kuwafikisha mbele ya sheria watenda jinai?
Amesema katika kujibu
swali lake hilo, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
alimueleza kuwa, anayo majina ya wale wote waliohusika na mashambulizi
ya Februari 5, lakini hakuna yoyote atakayewatia mbaroni.
Waislamu wamekuwa wakishambuliwa na
kuuliwa ovyo na wanamgambo wa Kikristo wa Anti-Balaka licha ya kuwepo
wanajeshi wa Umoja wa Afrika na Ufaransa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
0 comments:
Post a Comment